tiko
tiko
MSANII wa
filamu za Kibongo, Yusuf Mlela amefunguka kwamba baada ya kuishi
‘singo’ kwa muda mrefu, sasa anajipanga kuoa hivyo ndani ya mwaka huu
lazima ndoto yake hiyo itimie.
Akipiga stori na gazeti hili, Mlela
alisema mwaka huu amejiwekea malengo mengi lakini kubwa zaidi ni kuoa
kwani anahisi akiendelea kuwa peke yake kuna mambo atakwama kwa kuwa
hatakuwa na mtu wa kumshauri kwa karibu.
“Kiukweli maisha yenyewe ni mafupi na
umri nao unaenda hivyo lengo langu kubwa kwa mwaka huu ni kuoa na kuhusu
nitamuoa nani itajulikana baadaye lakini kwa sasa tambueni kwamba mwaka
huu lazima nioe, nimechoka maisha ya ubachela,” alisema Mlela ambaye
ameingia kwenye Top 3 ya Ijumaa Sexiest Bachelor kwa mwaka 2014-15.
tiko
tiko
Post a Comment