tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Waandamanaji wakichoma matairi ya magari
Polisi
katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili
kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu
Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.
Serikali
inasema kuwa watu wanne walifariki katika vurugu za Jumatatu ingawa
upinzani unasema idadi huo huenda ikawa juu kuliko iliyonakiliwa.
Wanafunzi
wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhudiwa wakichoma magurudumu,
katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.
Wanatuhumu
wanasiasa wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila ambaye muhula wake wa
pili unatarajiwa kumalizika mwaka ujao kwa kujaribu kujiongeza muda
mamlakani kwa kuidhinisha mipango ya kufanyika sensa ambayo
itachelewesha uchaguzi kwa miaka mingi.
Vurugu
hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda
ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.
Vijana walioandamana kwa vurugu, waliteketeza magurudumu ya magari, kupora maduka na kurusha mawe.
Wanafunzi waliambia BBC kuwa polisi walivamia chuo chao baada ya wao kuanza kuandamana.
Walisema polisi waliingia katika vyumba vyao na kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi.
Viongozi
wa upinzani walitoa wito kwa waandamanaji kwenda barabarani kupinga
mipango ya serikali kumuongeza muda zaidi mamlakani Rais Joseph Kabila
huku wakiutaja mpango huo kuwa mapinduzi ya kikatiba.
Mswada huo unapendekeza kufanyika sensa kote nchini ambayo itachukua kipindi cha miaka mitatu.
Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001. Muhula wake wa pili unakamilika mwaka 2016 kikatiba.
via>>BBC
via>>BBC
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment