tiko
tiko
VIJANA
watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani
CHADEMA, wamekamatwa na polisi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es
Salaam leo Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya jaribio lao la kufanya
matembezi kutoka mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona
Rais Jakaya Kikwete kufikisha malalamiko yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu,
Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na
maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya kuwasili kwenye eneo lake la
utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini
walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya
watembee safari ndefu kama hiyo?
DC
Rugimbana alisema, walimweleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili
wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna
hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kw amatumizi mabaya
ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya
raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.
Baada
ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya
kumuona Rais wa nchi, hata hivyo sio kumuona kiholela bali ni kwa
utaratibu maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari
walikuwa wamevunja sheria lakini akawataka wasubiri awasiliane na
wakubwa ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais.
Hata
hivyo vijana hao walikataa na walipotoka nje ya ofisi ya DC hapo
Kinondoni, walifanya tena jaribio la kuelekea Ikulu na safari hii polisi
hawakufanya masihara, waliwaweka chini ya ulinzi mita chache kutoka taa
za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa
ukiwa uneelekea Kariakoo.
Vijana hao wakiwa kwenye safari yao eneo la Magomeni Kagera
Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakielekea kituo cha polisi Magomeni Mapipa
Polisi wakionye raia kutounga "tela" safari ya vijana hao wakati wakiwa eleo la Magomeni Mwembechai
Polisi wakimdhibiti mmoja w avijana wasiokubali "kupitwa"
Polisi wakiwahi kukamata vijana
Vijana wakiwa chini ya ulinzi
Wakionyesha mshikamani baada ya kukamatwa
Mkuu
wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana,
akiwaeleza waandishi wa habari matokeo ya mazungumzo yake na vijana hao.
tiko
tiko
Post a Comment