tiko
tiko
Kwa
muda wa takribani wiki mbili kumekuwepo na habari juu ya kuvunjika kwa
mahusiano ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo na
mrembo/mwanamitindo Irina Shayk.Mapema wiki iliyopita msemaji rasmi wa Irina Shayk alithibitisha kwamba mrembo huyo wa kirusi ameachana na Ronaldo ambaye alikuwa na mahusiano nae ya muda wa miaka 5, hata hivyo tetesi juu ya chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano huyo zikaendelea huku mama mzazi wa Cristiano Ronaldo akitajwa kuhusika.
Mama mzazi wa Ronaldo, Dolares ametajwa kumkataa Irina kwa sababu haoni kama mwanamke huyo atafaa kuwa mzazi mwema kwa mtoto mdogo wa Ronaldo aitwaye Cristiano JR.
Hata hivyo baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye Cristiano Ronaldo ameibuka na yeye amethibitishwa kwamba ameachana na Irina huku akiomba sasa jamii imuache na maisha yake binafsi.
Katika taarifa aliyotoa leo kwa vyombo vya habari, Ronaldo alisema: “Ni kweli uhusiano wangu wa miaka mitano na Irina umefikia tamati. Kuachana ni uamuzi ambao tuliufikia wote wawili na kitu ambacho tunaamini ni sahihi kabisa kukifanya kwa sasa.
“Natoa taarifa hii ili kumaliza maneno maneno juu ya maisha yangu binafsi,” – alimaliza Cristiano Ronaldo.
tiko
tiko
Post a Comment