tiko
tiko
Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki
Sanga,amesema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwa sababu wazazi wake
wamemtolee nje ishu ya kwenda kumposa staa wa kike Bongo, Jacqueline
Wolper.

Msanii wa filamu hapa Bongo, Manaiki Sanga akiwa na Jacqueline Wolper.
Akizungumza kwa masikitiko, Manaiki
alisema kuwa hivi karibuni alifunga safari na kwenda kijijini kwao Mbeya
kwa ajili ya kuwaeleza wazazi wake nia yake ya kumuoa Wolper lakini
imekuwa tofauti kwani wamemwambia kama anataka kuoa msichana atatoka
nyumbani kwao.
“Yaani nimeamini kabisa mbio za sakafuni
huishia ukingoni, sikujua kama wazazi wangu watanikata maini kwa kuwa
nilijua wazi hawatakuwa na kipingamizi lakini wameniambia kuwa lazima
nioe nyumbani,” alisema.
tiko
tiko
Post a Comment