tiko
tiko
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja.
Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jasson Rweikiza, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya aliyekuwa akiishikilia nafasi hiyo, William Ngeleja, kujiuzulu.
Ngeleja,
ambaye ni Mbunge wa Sengerema (CCM), alijiuzulu nafasi hiyo, kutokana
na kuhusishwa na kashfa ya kupata mgawo kutoka katika fedha zilizochotwa
kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT).
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alithibitisha jana bungeni, kuhusu Rweikiza kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Hata
hivyo, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) alisema jana kuwa
amesikitishwa sana kumpoteza Ngeleja kama mwenyekiti wa kamati hiyo.
“Hii
haina uhusiano na masuala yake ya Escrow na siyo utetezi wa
aliyoyatenda na aliyoacha kuyatenda kuhusiana na sakata la Escrow. Ubora
wake kwenye kamati siyo utetezi wa makosa yake ya Escrow,” alisema
Lissu, ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo.
Alisema
Ngeleja aliongoza kamati hiyo vizuri na kuijengea heshima kubwa tofauti
na mtangulizi wake, Pindi Chana, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Lissu alisema chini ya uongozi wa Ngeleja walijadili miswada ya sheria na kupokea maoni ya wadau na kuyafanyia kazi vizuri.
“Na
kwa sababu hiyo, quality ya taarifa za kamati iliongezeka sana hata
ubora wa maoni ya wadau uliongezeka sana. Ngeleja ameiunganisha kamati
kweli kweli. Wakati wa Chana kamati iliongozwa na mkono usioonekana.
Kilichokuwa kimezungumzwa kwenye kamati sicho kilichokuwa kinaingizwa
kwenye taarifa tofauti na wakati wa Ngeleja,” alisema Lissu.
Aliongeza:
“Kwa hiyo, kipindi cha Ngeleja kilikuwa kizuri sana. Mimi nimesikitika
sana kumpoteza Ngeleja kama mwenyekiti wa kamati.”
Wajumbe wengine waliomsifu Ngeleja, ni Ali Khamisi Seif (CUF), Rukia Kassim (CUF) na Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi).
tiko
tiko
Post a Comment