tiko
tiko
Jeshi
La Polisi limetoa sababu za kwanini lilizuia maandano ya wafuasi na
viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kwamba ni kutokana na kuibwa kwa
bunduki saba katika kituo cha Polisi Ikwiriri wilayani Rufiji, mkoani
Pwani ambazo pengine zingeweza kutumika katika mkusanyiko wa watu.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, akihojiwa
jana na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) alisema jeshi hilo
liliwasihi tangu awali viongozi wa CUF kwamba wasifanye maandamano
kutokana na kuwapo kwa taarifa kuwa silaha zilizoibwa Ikwiriri
zingetumika pengine katika maandamano hayo.
“Tuliwaeleza
kuna silaha ambazo zimeibwa Ikwiriri na hatuwezi kujua zitatumika
maeneo gani, lakini kuna uwezekano zikawa zimeingia Dar es Salaam, hivyo
tukawaambia hizi silaha hatuwezi kujua zitapiga wapi na zitakuwa na
madhara gani,” alisema Sirro.
Kamanda
Sirro alisema sababu nyingine ambayo CUF walielezwa ni kwamba katika
mauaji ambayo yalifanyika Pemba pia wapo askari polisi waliouawa, hivyo
taarifa ambazo jeshi hilo lilikuwa limezipata ni kwamba maandamano hayo
yasingeweza kwisha salama.
Juzi
Jeshi la polisi lilitumia nguvu kwa kupiga mabomu na silaha za moto
wakati wa kuwakamata wanachama wa CUF waliokuwa wamekusanyika baada ya
jeshi hilo kuwazuia wasiandamane kufanya kumbukumbu ya wanachama wa
chama hicho waliouawa na Jeshi hilo mwaka 2001.
tiko
tiko
Post a Comment