tiko
tiko
SELEMANI Msindi,
ndiye msanii wangu bora kabisa wa tungo za kiume, zinazopeleka ujumbe
moja kwa moja pasipo mafumbo na kama itabidi liwe fumbo, kwa wanazuoni,
ni rahisi mno kujua mlengwa.
Wengi wanamfahamu kama Afande Sele,
kijana wa pale Morogoro ambaye wakati f’lani akitafuta maisha, aliwahi
kujaribu kupata ajira katika Jeshi la Polisi, chanzo hasa cha jina lake
hili la kisanii. Kati ya wasanii wakubwa ninaowafahamu kwa karibu
kupitia kazi zao, huyu naye yumo!
Kitu kimoja kizuri ni kwamba Afande Sele
anajua vizuri lugha ya Kiswahili, ndiyo maana tungo zake zimekuwa
kielelezo cha msanii makini anayejua nini anaimba, kwa ajili ya nani na
kwa wakati gani.
Haikuwa ajabu alipotwaa taji la Mfalme
wa Rhymes katika shindano la pekee kuwahi kufanyika nchini. Nimefanya
naye kazi kwa ukaribu, ninamfahamu kwa kiwango cha kuridhisha. Ingawa ni
mtu makini akiwa nyuma ya mic, nje ya fani Afande anabaki kuwa mswahili
tu kama tulivyo waswahili wote, anacheka na kila mmoja na anawang’ong’a
kila wakimpa kisogo!
Ingawa mimi ni shabiki wa kweli wa
Afande, mtu ninayemkubali sana, huenda kwa sababu ya kuwa naye karibu
kikazi, nimegundua tatizo lake moja la msingi, kuna wakati, kwa sababu
anazozijua mwenyewe, huamua kuikwepa nafsi yake inayojulikana na
kujivika asiyokuwa nayo.
Kwa hili, nimewahi kutofautiana naye
mara kadhaa na ninachoshukuru, hakikuwahi kuharibu ukaribu wetu. Afande
anasema asichotenda na anatenda asichosema! Wote tunajua, wasanii wengi
wa muziki wa kizazi kipya wamejitumbukiza katika utumiaji wa madawa ya
kulevya (Cocaine na Heroin) na wapo rafiki na ndugu zetu wamepoteza
maisha kwa kuhusishwa na jambo hili, ingawa enzi za uhai wao, walikuwa
wakikataa katakata kujihusisha nalo.
Nimewahi kusema mara kadhaa, watu
hawawezi kumzushia mtu kitu kisichofanana na ukweli. Kwa mfano, tunao
watu, ambao ni marafiki zetu, ndugu zetu na hata wafanyakazi wenzetu,
wanatajwa kuwa ni mashoga, walevi, wezi na kadhalika. Hatuwezi kuamini
moja kwa moja, lakini pia hatuwezi kupuuza. Kwa nini watajwe wao na siyo
wengine?
Hatuna ushahidi, lakini utapuuza vipi
unaposikia kila siku watu wanawataja Banzastone, Msafiri Diouf, Chid
Benz, TID, Lord Eyez, Ray C na wengine kuwa wanakula ‘sembe’?Juzi,
nimesoma mahali, mshkaji wangu Afande Sele akimtetea Daz Baba, yule
mkali kutoka Kundi la Daz Nundaz, aliyetamba na vibao vingi vikiwemo
Umbo Namba Nane, Elimu Dunia na kadhalika, kwamba kudhoofika kwake mwili
hakutokani na utumiaji wa madawa ya kulevya, bali ni unywaji pombe
uliopitiliza.
Ninamfahamu Daz Baba na ninajua Afande
na Daz Nundaz ni washkaji. Anachofanya ni kujaribu kupooza sauti
isiyokoma, inayopaza kuwa bwa’ mdogo anakula unga. Kama nilivyosema
mwanzo, hatuna ushahidi, lakini kwa nini tupuuze sauti hii, inayotolewa
na watu wanaomfahamu?
Kumsaidia Daz Baba na wengine wanaotajwa
ni kuwaambia ukweli kuwa wanapoteza mwelekeo. Tuwaambie kuwa
wanachokifanya sasa ni ujanja wa kizamani, ambao umewapoteza watoto
wengi wa Kariakoo, Magomeni, Kinondoni, Mwananyamala, Ilala na Temeke,
ambao leo hii wamekuwa ombaomba kwa watu ambao wakati wanaingia mjini
kutafuta maisha, wao waliwaita wakuja!
Kwa hiyo ningetegemea Afande Sele, siku moja aachie kibao kinachowataja washkaji zake wabwia unga, akiwataka waache, kwa ajili ya Tanzania salama!
Kwa hiyo ningetegemea Afande Sele, siku moja aachie kibao kinachowataja washkaji zake wabwia unga, akiwataka waache, kwa ajili ya Tanzania salama!
tiko
tiko
Post a Comment