tiko
tiko
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ameibuka na kutamka yeye
si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema
amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa
waimbaji wengine.
Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa
vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa
Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokanana nafasi yake
katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.
Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio
ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la
Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda
mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose.
“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi
ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba
pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika
na kushindwa kutokea.
“Lakini, naomba watumishi wa Mungu
wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi
ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.
“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha
anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama
katika taarifa hiyo na kuongeza:
“Agosti mwaka huu, kampuni yangu
ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na
maana kwamba ni Meneja wake.
“Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko
Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini
hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa
wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.
“Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha
la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na
tulishamlipa,” alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe
na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.
Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji
huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa
baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana
yeye ndiye amemzuia.
“Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya
Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu
hilo,” alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika,
angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.
Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai
ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona
akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti
na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.
“Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika
ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu
mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye
kujielewa,” alisema Msama.
Rose ni mwimbaji mahiri wa muziki wa
injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya ukanda wa Afrika
Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkatabawa kufanya
kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini.
Miongoni mwa albamu zilizompa umaarufu
Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa injili nchini, ni
‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa,
Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu
aliyoachia hivyo karibuni.
Chazo:Jiachie
tiko
tiko
Post a Comment