tiko
tiko
JESHI
la Polisi limesema linaendelea na msako mkali wa kuwabaini watu
wanaodaiwa kuhusika na tukio la kuuawa kwa askari polisi wawili wilayani
Rufiji.
Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi, walivamia Kituo cha Polisi Ikwiriri ambapo waliua askari wawili na kuiba silaha.
Akizungumza na paparazi, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, alisema pamoja na kuendelea na kazi hiyo, lakini kwa sasa hawezi kuzungumza kwa undani tukio hilo kwani anaweza kuharibu mwenendo wa uchunguzi.

“Kwa kweli siwezi kusema lolote kuhusu operesheni hii kwa sababu tunaweza kuharibu upelelezi wetu, hivyo kuweni wavumilivu tutakapokamilisha tutatoa taarifa kwa vyombo vya habari ili wananchi watambue tulichokipata katika uchunguzi wetu,” alisema Chagonja.
Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ameahidi kutoa zawadi ya Sh milioni 20 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa na hatimaye kupatikana kwa silaha zilizoporwa na majambazi hao.
Tukio hilo lilitokea Januari 20 saa nane usiku katika Kituo cha Polisi Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani ambapo askari wawili; Koplo Edgar ambaye alikatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi katika ubavu wa kulia na kutokea upande wa kushoto wote walifariki dunia.
tiko
tiko
Post a Comment