tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Stori: Musa Mateja
BAADA ya
kuwa na malengo ya kuolewa mwaka 2014, mwigizaji Elizabeth Michael
‘Lulu’ ameibuka na kusema imeshindikana lakini hajilaumu wala hamlaumu
mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye
anayewezesha kila kitu.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Lulu alisema mwaka 2014
alikuwa na malengo mengi likiwemo suala la ndoa lakini kwa kuwa Mungu
ndiye muweza, atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.
“Ndoa ni mipango ya
Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu huwa tuna
mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu,”
alisema Lulu.
Akizidi kupiga stori na
paparazi wetu, Lulu alisema kwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka
malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala
la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo.
“Sina mpango hata kidogo
kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita ndiyo
ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.
Alipotakiwa kumtaja
mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kufunguka lakini akakubali
kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.
“Kwanza nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na
mapenzi ya kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth
pekee. Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa,” alisema Lulu.
Kuhusu mikakati yake ya
sanaa mwaka huu, Lulu alisema ana mpango wa kuendelea na masomo huku
akiwa pia na ‘project’ kubwa mbili ambazo anatarajia kuzifanya.
“Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana nitaziweka wazi,” alisema Lulu.
tiko
tiko
Post a Comment