tiko
tiko
WAENDESHA magari ya kusafirisha abiria
katika ya Jiji la Mwanza maarufu kama daladala leo wamefanya mgomo na
kuziba njia zote zinazoingia mjini kutokana na maeneo waliyokuwa
wanaegesha magari yao kwa ajili ya kusubiri abiria (stendi) kugawiwa
wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga kwa aijili ya
shuhuli zao.
Hali hiyo imetokea leo asubuhi katika
eneo la Stendi ya Tanganyika na Stend ya Soko Kuu jijini Mwanza ambapo
yanaegesha magari ya kwenda Airport, Ilemela, Bwiru na Mwaloni ambapo
madereva hao waliziba njia zote zinazo ingia kwenye maeneo hayo.
Mwenyekiti wa waendesha daladala Mkoani
Mwanza, Hassan Dede Petro alisema hali hiyo imejitokeza kutokana na
wafanyabiashara hao kuanza kugawana maeneo kwenye stendi hizo bila
uongozi wa waendesha daladala kuwa na taarifa yeyote kuhusu suala hilo.
''Hali hii imejitokeza kwa sababu ya
wafanyabiashara wadogodogo kuanza kujigawia maeneo katika eneo letu
ambalo tunaegesha kwa ajili ya kusubiri wateja wetu (abiria)'' Alisema
Petro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
wafanyabiashara ndogondogo 'machinga' Said Tembo alisema walichukua
uamuzi huo kutokana na kupata ruhusa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Mhe. Magesa Mulongo kuwa watumie maeneo hayo kwa shuhuli zao za
kufanyabiashara kwenye maeneo ya stendi hizo.
tiko
tiko
Post a Comment