tiko
tiko
KLABU ya Manchester City imepokea kipigo
cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wake wa
Etihad jijini Manchester leo.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya
England, mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Santi Cazorla kwa penalti
huku la pili likifungwa na Olivier Giroud kwa kichwa.
Kwa matokeo ya leo, Manchester City
imeendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 huku ikiwa na pointi
5 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea wenye pointi 52. Asenal wapo
nafasi ya tano wakiwa na pointi 39.
tiko
tiko
Post a Comment