tiko
tiko
Taarifa
iliyotolewa na jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es salaam, imesema kuwa
katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa kwa risasi wakati wakijaribu
kuwadhuru askari.
Tukio
hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Livingstone saa
3.00hrs usiku. Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na mlalamikaji
alikuwa anatumia taa za kawaida.
Mara
baada ya kuanza tukio hilo la uporaji wasamaria wema walijulisha Jeshi
la Polisi ndipo kikosi maalum cha kupambana na majambazi (ant robbery
squared) kilipofika kwa haraka katika eneo la tukio tayari kwa
mapambano.
Taarifa
hiyo inasema kuwa Majambazi hao walistuka na kuanza kuwarushia risasi
askari waliokuwa katika gari la Polisi na ndipo sasa kukawa na mapambano
ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa kutumia silaha na
kurushiana risasi. Hatimaye majambazi wawili waliuawa mmoja
anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O
OCHENG @ ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya.
OCHENG @ ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya.
Jambazi
mwingine aliyeuawa ametambuliwa kwa jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB,
Miaka 46, Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Majambazi
wengine waliotoroka baada ya tukio hilo wanaendelea kutafutwa na
tunaomba raia wema waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili
wapatikane.
Pamoja
na kuuawa kwa majambazi hawa na kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa
pikipiki mbili moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249 CMC, rangi
nyekundu. Nyingine ni aina ya BOXER yenye namba za usajili MC350 AM
rangi nyeusi ambazo zote zilitumiwa na majambazi hao katika tukio.
Aidha, Jambazi ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya TECNO.
MAJAMBAZI WENGINE TISA SUGU WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM
Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Oparesheni
kali bado inaendelea jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha kwamba
majambazi wote wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine ambayo ni kero
katika jamii yanashughulikiwa kikamilifu. Pamoja na mafanikio hayo
tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao za kutoa taarifa mapema
zenye kuwa na mafanikio ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee
kuwashwari.
tiko
tiko
Post a Comment