tiko
tiko
Mikoa ya mtwara na lindi iko hatarini kuingia gizani kutokana na kiwanda kilichopo msimbati kinachotumika kuchakata gesi inayotumika kufua umeme katika mikoa hiyo sehemu ya ardhi yake mita miamoja na sita, kumezwa na maji ya bahari na kubakia mita 25 kufika eneo la kiwanda.
Akizungumza
na vyombo vya habari katika eneo la tukio naibu waziri nishati na
madini mheshimiwa CHARLES KITWANGA amesema tukio hilo limetokana na mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha katika nchi za malawi na msubiji na hivyo
kuleta madhara upande wa tanzania.
Katika
kukabiliana na hilo naibu waziri amelazimika kuitisha kikao cha dharura
cha kamati ya ulinzi na usalama na kuona njia rahisi ni kutumia jeshi
la majini na nchi kavu ili kusaidia kuzuia sehemu ya kiwanda iliyobaki
isimezwe na maji.
Huku
muhandisi mkuu wa kiwanda hicho cha M and P PETER JOHN akisema endapo
ardhi hiyo itaendelea kumegwa wakati wowote watasitisha kazi ili
kunusuru maisha ya watu na mali zinazohamishika.
Mbali
na kiwanda hicho pia bomba kuu la gesi linalotoka baharini na
kuisafirisha gesi katika viwanda vya mtwara na lindi na hatimaye dar
kinyerezi kwa ajili ya kufua umeme wa gredi ya taifa nalo liko hatarini
kuadhirika kwani bahari imebakiza mita sita kufikia eneo la nchi kavu
lilipo bomba hilo.
Dhoruba
hiyo imetokea usiku wa tarehe 13 kuamkia tarehe 14 ambapo kipande cha
ardhi chenye ukubwa wa mita miamoja na sita kiliweza kumezwa na maji ya
bahari kwa muda wa masaa matatu.
tiko
tiko
Post a Comment