tiko
tiko
Huu ni ubunifu ambao hata mimi umenivutia, nakumbuka mwaka 2012 rapper Jay Z aliwahi pia kusurprise
kwa kuingia kwenye treni ya abiria halafu akaendelea na safari, huku
aliyekaa naye kiti kimoja alikuwa bibi mzee ambaye hata hakujua kwamba
amekaa na staa mkubwa duniani!
Maria Carey
naye amekuja na hii kwa fans wake Las Vegas, mashabiki wake walikuwa
wakihojiwa ndani ya vyumba vya hoteli, wakaeleza namna ambavyo
wanamkubali staa huyo, halafu ghafla mlango unagongwa na mtu ambaye
anajitambulisha kuwa ni mhudumu wa hoteli, halafu wanapogeuka
kumuangalia mhudumu wanakuta mhudumu huyo ni Maria Carey mwenyewe!
Hii imenivutia, katika surprise hiyo
fans wake hao walipata nafasi ya shavu la ticket za show yake ambayo
ataifanya May 6 Las Vegas, Marekani.
“Hili ni tukio muhimu kwangu na
tena nina imani mashabiki wangu wataifurahia hii kwa sababu naenda
kufanya shoo ambayo ni kama njia ya kuiongoza album yangu ambayo ni
toleo la 18, naamini watu wengine watafurahia kwa sababu sijawahi
kufanya hivi kabla“ — Mariah Carey.Video na pichaz za surprise hiyo ziko hapa.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment