tiko
tiko
Mwili
huo uligundulika majira ya saa sita mchana baada ya watu waliopita
katika eneo hilo kuuona ukiwa umelazwa karibu na moja ya shamba lililopo
mtaa wa Bunkango eneo la kambi hiyo ya Polisi.
Paparazi ilishuhudia mwili huo ulioanza kuharibika ukiwa umevuliwa nguo zote ukiwa bado haujaondolewa katika eneo hilo la tukio.
Mwili huo ulikuwa na majeraha maeneo ya usoni kiasi cha kushindwa kutambulika kirahisi.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo, Kaimu Mtendaji wa
kata ya Nshambya, Christian Ngaiza, alisema alipata taarifa za tukio
hilo kutoka kwa dereva wa bodaboda kuwa kuna mtu ameuawa lakini wananchi
wanaogopa kutoa taarifa Polisi.
Ngaiza,
alisema baada ya kupata taarifa hiyo aliamua kwenda eneo la tukio
majira ya saa saba mchana na kutoa taarifa ya tukio hilo Polisi.
Aidha,
alisema baada ya kubaini mwili huo, alianza uchunguzi na kuhoji
wananchi wa mitaa yote mitatu ya eneo hilo endapo wana taarifa za mtu
yeyote aliyepotea ambapo ilibainika hakukuwa na mtu aliyepotea
Mkazi
wa Mtaa wa Migera, Joyce Nuru, akizungumzia tukio hilo, alisema alipata
taarifa za kukutwa kwa maiti huyo, akiwa nyumbani kwake ambapo majira
ya saa sita mchana wanafunzi walipita na kumueleza kuwa kuna mtu
amekufa maeneo ya mnara.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ambaye pia ni mpelelezi wa makosa ya
jinai mkoani humo, Gilles Mroto alisema tukio hilo amelisikia na
ametuma timu ya maofisa wa Polisi kwenda eneo la tukio kufanya
uchunguzi.
Hata hivyo, mwili huo haukuweza kutambulika na hivyo kuzikwa na Manispaa ya Bukoba katika makaburi ya Kyebitembe.
tiko
tiko
Post a Comment