tiko
tiko
Mbuzi wakiwa wamezibwa midomo.
KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni
ubunifu wa hali ya juu, mfugaji mmoja, Msimbe Jonas wilayani Mvomero,
Morogoro amebuni mbinu mpya ya kuzuia mbuzi wake kuingia katika mashamba
ya wakulima na kula mazao yao.
Mwandishi wetu aliyekuwa Mvomero
vijijini hivi karibuni alishuhudia Jonas akiwa na mbuzi wake ambao
amewatengenezea chombo (plastiki) na kuwafunga midomo yao ili kuwazuia
kula mazao katika mashamba ya watu.
...Wakiwa na makopo midomoni.
“Nimebuni mbinu hii ya kuwazuia mbuzi
wangu kula mashamba kwa kuwafunika midomo. Huwa naenda nao hivi hadi
mbali kabisa na mashamba ya watu, huko nawafungua ili wale majani,
wameshazoea,” alisema Jonas.
Aliongeza kwamba mbinu hiyo ni nzuri na
imemfanya asiwe na wasiwasi anapopitisha mbuzi wake karibu na mashamba
ya wakulima.“Baadhi ya wakulima walioona mbuzi wangu wakiwa hivi
wamefurahia sana ubunifu wangu huu,” alisema Jonas.
tiko
tiko
Post a Comment