tiko
tiko
Idara ya polisi ndio taasisi
inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi
katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Ripoti hiyo inasema kuwa
maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa
wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka uliopita.
Ya pili ni idara ya
mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia mfukoni asilimia 18 ya
hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na utoaji wa leseni
yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.
kwa mujibu wa gazeti la The
Citizen, Idara ya Polisi nchini Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa
ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.
Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.
Utafiti huo ulifanywa mwezi
Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye na maslahi ya
kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana na Jukwaa la uwazi
nchini tanzania Trafo.
BBC SWAHILI
tiko
tiko
Post a Comment