tiko
tiko
Mabosi na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika tambiko hilo linalodaiwa kufanyika mapema wiki hii.
Za kitaa kutoka Mtwara zinadai kuwa bibi
mmoja aliyeitisha Serikali kuwa ikifanya mchezo na haki za watu wa mkoa
huo atabadili gesi kuwa maji, amewapigia tambiko Wafaransa wazungu wa
Kampuni ya uchimbaji wa visima vya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd
yenye ofisi zake Chole Road,
Msasani Peninsular, Dar es Salaam, baada ya kile kilichodaiwa drill yao
ya kuchimbia mafuta kukatika mara tatu wakati wakichimba kisima cha
urefu wa mita 3,000 chini ya bahari. Inadaiwa baada ya kuanza kuona
maajabu katika kazi yao hiyo, fasta walijisalimisha kwa bibi huyo huko
Mtwara na kukubali kufanyiwa tambiko ili mambo yanyooke, kama
wanavyoonekana pichani hapo juu! Kama ni kweli, basi bibi anatisha!
Lol!!.
PICHA: Hisani ya Mtandao
tiko
tiko
Post a Comment