Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

EPL: Chelsea vs Man City – wamekipiga leo matokeo haya hapa

tiko tiko
(null)
Baada ya Liverpool na Manchester United kupata ushindi jioni ya leo – vilabu vingine vikubwa kwenye ligi kuu ya Uingereza Chelsea na Man City navyo vilikuwa vikichuana katika vita kugombea uongozi wa ligi hiyo.
Mechi hiyo ambayo ilipigwa jijini London katika dimba la Stamford Bridge imemalizika muda mfupi uliopita huku Chelsea wakiweza kuendelea kuustawisha uongozi wao kwenye msimamo wa ligi.
Matokeo ya mechi hiyo ni sare ya 1-1 ambayo imeendelea kuipa Chelsea uongozi wa pointi 5 zaidi ya Man City wanaoshika nafasi ya pili.
Chelsea walianza kufunga goli kupitia Loic Remy ambaye alimalizia kazi nzuri ya Eden Hazard katika dakika ya 40 – lakini muda mfupi baadae David Silva akaisawazishia City baada ya kumalizia pasi ya Sergio Aguero.
Mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa yakisomeka 1-1.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top