tiko
tiko
WATANGAZAJI ambao
walikuwa wanandoa kabla ya kuachana, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden
Jumanne wamemaliza tofauti zao na sasa wamekuwa marafiki sana kiasi cha
kuzua minong’ono kwamba wamerudiana.
Watangazaji, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne wakati wakiwa wanandoa.
Baada ya minong’ono hiyo kuzidi, Risasi
Vibes ilimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alisema ni kweli
amemaliza bifu na Ezden na sasa ni marafiki lakini suala la kurudiana
siyo kweli na halipo kabisa kwani tayari yeye ana mtu wake na Ezden pia
ana mtu wake.
“Tumemaliza vinyongo tulivyokuwa navyo
na sasa tuko kama watu wa kawaida lakini hakuna mapenzi tena na hatuwezi
kurudiana. Pia kila mtu ana uhusiano mwingine, sisi ni marafiki tu watu
waelewe hivyo,” alisema Dida.
tiko
tiko
Post a Comment