Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

BREAKING NEWS:MMOJA WA PANYA ROAD AUWAWA MAENEO YA UKONGA MOMBASA KWA DIWANI AMBAPO MWILI WAKE BADO HAUJACHUKULIWA NA POLISI MPAKA SASA

tiko tiko
 

Umati wa watu wakishuhudia.

Polisi wakibeba mwili wa marehemu.

Mwili ukipakiwa garini.

Polisi wakisubiri gari ilikumchukuwa marehemu.

Askari wakiandaa gari ili kupakiwa mwili wa marehemu.

Kibaka maarufu kama mbwa mwitu aliyeuwawa na  wananchi wenye hasira kali.

Kufuatia tabia ya vijana kuuunda makundi ya uharifu na kuvamia nyumba au watu mchana kweupe na kufanya vitendo vya uporaji na kupiga huku wakijibatiza majina kama vile mbwa mwitu na panya road,Kibaka mmoja amejikuta akiuwawa na kundi la wananchi mwenye hasira kali.

Ishu nzima ilitokea baada ya  vijana hao kuiba  pikipiki  juzi ya jamaa mmoja na wakati wakiwa wanaondoka ndipo mmoja wa vibaka hao alipodondoka na wananchi kumshambulia kwa kumpiga na kufa.

Mazishi ya kibaka huyo yalifanyika leo na ndipo kundi kubwa la mbwa mwitu wapatao 20 na kuendelea walipovamia makazi ya watu kwa kuingia kila nyumba kwa kupora mali zao ikiwa ni pamoja na kuwapiga jambo lililowakasirisha wakazi wa Kigogo Sambusa na kuamua kuwavalia njuga na ndipo walipomkamata  kibaka mmoja na kumuua.
PICHA ZOTE NA Gabriel Ng’osha/GPL
KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.

Maeneo yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi.
Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana leo baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.

Baada ya kumzika mwenzao leo, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo.
Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar.
Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa.
Wateja waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge walilazimika kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine wakikanyagana na kukatwa na vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa vijana hao walikuwa wanakatiza maeneo hayo japo hawakuingia ndani.

Baada ya tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi yao kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia.
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top