tiko
tiko
Taarifa
iliyotufikia asubuhi hii,inaeleza kuwa majambazi yamevamia kituo cha
Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora
silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza
maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi
ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
Hivi
sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi
wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika Tukio la uvamizi, kituo cha polisi
Ikwiriri, Rufiji, Pwani
Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabom ya machozi na risasi 60 za smg.
tutaendelea kujuzana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.
tiko
tiko
Post a Comment