tiko
tiko
EMMANUEL NELSON mwenye
umri wa miaka kati ya (30 au 35, ambaye ni mzaliwa wa Mbamba Bay,
Ruvuma, na ambaye wazazi wake wanaishi Dodoma, anaomba msaada wa
kutibiwa taya ambalo limevunjika.
Nelson ambaye alishindwa kuongea akiwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alifikishwa na polisi wa
kituo kidogo cha Pangani, Ilala, jijini Dar es Salaam, Januari 15,
mwaka huu baada ya kumwokota barabarani, anasemekana alivunjwa taya hilo
kwa kupigwa na watu wasiojulikana.
Mtu huyo ambaye amelazwa katika wodi ya
Sewa Haji namba 23, amesema ameshindwa kupata Sh. 60,000/= kwa ajili ya
gharama za matibabu na kulazwa ambapo amesema ametelekezwa na ndugu zake
wanaoishi Tabata-Relini, jijini Dar es Salaam.
Nelson anahitaji kufungwa waya na matibabu mengine ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
Kwa yeyote aliyeguswa na tukio la mgonjwa anaweza kumchangia kupitia namba ya simu 0655 207 156, pia anaomba ndugu, jamaa na marafiki wajitokeze kumwona na kumsaidia.
Kwa yeyote aliyeguswa na tukio la mgonjwa anaweza kumchangia kupitia namba ya simu 0655 207 156, pia anaomba ndugu, jamaa na marafiki wajitokeze kumwona na kumsaidia.
tiko
tiko
Post a Comment