Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Amuua mkewe kwa risasi na kisha kujiua mwenyewe wakiwa kituo cha Polisi

tiko tiko
images (1)Mara nyingi kituo cha Polisi ni mahali ambapo mtu anakuwa na uhakika wa kuwa na usalama, kuna matukio yakitokea katika maeneo hayo huwa ni ya kushtua, mojawapo ni kama hili la mwanaume mmoja kumuua mke wake na kisha kujiua mwenyewe wakiwa katika kituo cha Polisi cha Parkview, Johannesburg Afrika Kusini.
Mtu na mkewe walifika katika kituo cha Polisi kwa ajili ya kupeleka malalamiko ya mgogoro wa kifamilia waliokuwa nao, wakiwa wanatoa maeleo kila mmoja, mwanaume aliomba akachukue miwani yake ya kusomea katika gari, aliporudi alikuja akiwa na bastola, akampiga mke wake na kumuua, kisha akawanyooshea askari waliokuwa zamu, mwisho akajiua mwenyewe.
Watu hao walifikishwa katika kituo cha Polisi wakiwa katika magari tofauti, walikuwa na ugomvi katika nyumba yao Johannesburg ambapo Polisi walifika na kuamua kuwachukua kwenda nao kituoni hapo ili wakatafute suluhu ya ugomvi huo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top