tiko
tiko
NAAM! kama
kawaida tumekutana tena kwenye kona yetu ili tujuzane machache,
tumeona wenyewe jinsi sikukuu ya Xmas ilivyokwisha, je mwenzangu
ulipata au ulipatikana. Nasikia wapo waliopombeka mpaka wakazimika, mmmh
makubwa watu wengine hawanywi mpaka sikukuu.
Hivyo unakunywa mpaka unazimika
unategemea nini, wenzako wakubebe eeh uwape shida kwa raha zako za
kijinga, haipendezi jamani kunyweni kadri ya uwezo wenu siyo lazima
kikiwa kingi basi lazima ukimalize. Kunywa na kula kwa uwezo wako.
Si unakumbuka nilikueleza nilivyomuokoa
mwanamke mlafi kila kitu kwake “hamu” yaani lazima kiingie mdomoni. Sasa
nisingetokea kama siyo siku ya pili kwenda kupigwa bomba ni nini,
tuacheni tamaa kwa kutaka kumkomoa mtu bila kujua mfukoni kwake yupo
vipi.
Matokeo yake ndiyo hayo unajidhalilisha
unakunywa mpaka unazimika, ya X-mas yamepita, sasa tuulizane sisi
wenyewe katika pitapita yetu ya kuchuna mabuzi, tumepata nini, je mwaka
huu ulikuwa wa faida au hasara kila siku kukopwa hata pesa ya sabuni
ya kufulia nguo ya ndani huna.
Usikubali kufanya kazi kwa kujifanya
ubao wa matangazo kila mwenye macho ajisomee utazeeka na ubakie
shangingi mstaafu mwenye sifa ya kukopwa na kupigwa mtungo tu, huna
lolote la maana!
Lazima sasa hivi tujiulize tumekwama wapi na kipi ulichokifanya kukuingizia kipato, usiwe wa kwenda kila siku hujui mwisho wa mwaka kazi yako imeingiza au imetoa.
Lazima sasa hivi tujiulize tumekwama wapi na kipi ulichokifanya kukuingizia kipato, usiwe wa kwenda kila siku hujui mwisho wa mwaka kazi yako imeingiza au imetoa.
Kama haina faida badili kazi nyingine
siyo lazima upigwe na baridi na kugeuzwa shamba la mbu bila faida.
Usiogope kujaribu biashara nyingine huenda ikakutoa na hiyo igeuke
starehe badala ya kazi.
Narudi kwako wewe wa ndani, umeumizwa
mara ngapi katika ndoa yako, umegundua kosa lako nini lililomfanya mumeo
asirudi mapema au kulala nje, au kazi yako kulia tu hujui lolote,
haipendezi lazima ujiulize iweje zamani alikuwa mapenzi motomoto leo hii
yamepungua na kuwa penzi la mgao kama umeme.
Kama utakuwa kimya kutegemea Mungu yupo nawe hujui matatizo yako talaka hiyoo unaiita mwenyewe.
Mwaka umekwisha, umegundua udhaifu wako. Hebu muda huu mchache utumie kujiuliza hata kukaa na mwenzako na kumuuliza mpenzi hebu nieleze kosa langu.
Mwaka umekwisha, umegundua udhaifu wako. Hebu muda huu mchache utumie kujiuliza hata kukaa na mwenzako na kumuuliza mpenzi hebu nieleze kosa langu.
Kwa vile ni mwisho wa mwaka kila mtu atatumia nafasi hii kuzika tofauti zake na kuingia mwaka na furaha na amani ya moyo.
Nawe uliyefanikiwa utumie mwaka huu kwa
mafanikio zaidi na kurudi ulikotoka, siku zote kufika kileleni ni rahisi
lakini kukaa kileleni ni kazi, ni wakati wa kuimarisha yote
uliyoyafanya mpaka ukajengewa nyumba au kununuliwa gari usibweteke gari
zuri likaozea uani.
Yangu ni hayo kwa mwaka 2014 na
kuwashukuru wote waliofuata, wengi wamefanikiwa na waliopuuza sasa
wanajuta. Si mwingine ni mimi anti Nasra Shangingi mstaafu. Heri ya
mwaka mpya.
tiko
tiko
Post a Comment