tiko
tiko
Mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye pia ni
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God jijini
Dar, Dk. Getrude Rwakatare (pichani) ameibuka na kusema hafikirii
kugombea nafasi hiyo mwakani.
Mbunge
wa Viti Maalum CCM ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la
Mikocheni B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare.
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini
Dar, Mama Rwakatare alisema amebaini kwenye siasa kuna watu wanataka
kutumia nafasi hiyo kumchafua jambo ambalo linampa wakati mgumu
ikizingatiwa kuwa ana watu wanaomwamini kiroho.
“Sifikirii kwa sasa kugombea ubunge
mwakani, siasa ina mambo mengi sana, bora niendelee kumtumikia Mungu,
kama wazo litanijia tena ni hapo baadaye,” alisema Mama Rwakatare.Mama
Rwakatare ambaye pia ni mmiliki wa Shule za St. Mary’s alisema anaamini
katika kumtumikia Mungu zaidi kuliko kujikita kwenye siasa.
Shule za St Mary’s zinazomilikiwa na Mchungaji Rwakatare zimekuwa juu kielimu karibu kila kona ya nchi.
Kwa mfano, Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International iliyopo Mang’ula, Ifakara, Morogoro imekuwa ya kwanza kiwilaya, St. Mary’s International Kihonda Morogoro Mjini imekuwa ya pili kiwilaya na ya tano kimkoa na imetoa mwanafunzi bora Afrika Mashariki wa kwanza katika mashindano ya insha.
Kwa mfano, Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International iliyopo Mang’ula, Ifakara, Morogoro imekuwa ya kwanza kiwilaya, St. Mary’s International Kihonda Morogoro Mjini imekuwa ya pili kiwilaya na ya tano kimkoa na imetoa mwanafunzi bora Afrika Mashariki wa kwanza katika mashindano ya insha.
Bado shule za St. Mary’s ziliendelea
kufanya vizuri kwani St. Mary’s Tabata jijini Dar ilikuwa ya sita
kiwilaya na wanafunzi wote walichaguliwa kuendelea kidato cha tano.
Shule ya St. Mary’s Mbagala ilishika
nafasi ya tano kiwilaya na wanafunzi wote wa darasa la saba
walichaguliwa. Shule ya St. Mary’s Mbeya ilikuwa ya pili kiwilaya na ya
sita kimkoa, mwaka jana ya kwanza kiwilaya na ya tatu kimkoa, watoto
wote walichaguliwa.
Mkurugenzi wa shule hizo, Mama Rwakatare
alisema shule zake zinafanya vizuri kutokana na kuwa na walimu wenye
sifa.“Walimu wote wana sifa, ndiyo kigezo tunachosimamia ili kuajiri.
Hii imetusaidia sana shule za St. Mary’s kuwa bora,” alisema mama
Rwakatare.
tiko
tiko
Post a Comment