tiko
tiko
IKIWA
imebakia siku moja kabla ya mwaka 2014 kumalizika, jiji la Dar es
Salaam limejikuta likigubikwa na mauaji ya mara kwa mara, hasa ya
kutumia silaha baada ya kubainika kuzagaa kwa bastola zilizo mikononi
mwa watu waovu.
Madaraka.
Silaha hizo sasa zimekuwa kama simu za
mikononi ambazo karibu kila mtu jijini Dar es Salaam anayo na hivyo
kuwapa hofu kubwa wananchi ambao hawajui lini na wapi litatokea tukio
la ujambazi, hasa kutokana na msongamano mkubwa wa watu.
Matukio mengi ya ujambazi yanayofanyika
nyakati za mchana kweupe, yanafanywa na majambazi ambao wanatajwa
kutumia pikipiki hasa aina ya Boxer, zinazoaminika kuwa na kasi kuliko
aina nyingine na usafiri ambao hauwezi kukwama kwenye foleni.
Baadhi ya matukio yanayomaliza mwaka na
kuzidisha hofu kwa watu ni kama lile lililotokea Tabata Kisukuru,
mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo kijana aliyetajwa kwa jina la
Mahamud Ally (19) kuuawa kwa kupigwa risasi na mtu mmoja anayedaiwa
kukerwa na kelele za majirani kwenye sherehe za send off.
Ilidaiwa kwamba mtu huyo hakupendezwa na
kelele hizo na mara kadhaa alitoka nje na kuwaamuru watu kukaa mbali na
nyumba yake, lakini hawakutaka kusikia. Alipoona watu wanakaidi,
anadaiwa kwenda kuchukua bastola yake na kuanza kupiga risasi ovyo
hewani, ambayo mojawapo ilienda kumkuta marehemu, ambaye alikuwa ni
mpita njia.
Ochola.
“Nakumbuka siku ya tukio majira ya saa
tano na nusu usiku nikiwa na wenzangu kwenye sherehe, tukijitayarisha
kukusanya vifaa vya muziki ili tufunge, ndipo jirani yetu alitoka
nyumbani kwake na kuanza kufyatua risasi ovyo, ya kwanza ilimpata
Mahamud kichwani na nyingine bega la kushoto akawa amedondoka chini,
risasi zilizidi kumiminwa na moja ikanipata shavuni,” alisema mmoja wa
majeruhi, aliyejitambulisha kwa jina la Goodluck.
Kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa
jina la Salim Ally alisema mdogo wake alikuwa na miezi miwili tu tokea
aje Dar kwa ajili ya kufanya kazi za ujenzi akitokea kwao Morogoro na
siku ya tukio, alikuwa ametoka kuachana naye kumsindikiza kwenda kulala.
Katika tukio lingine, huko Tabata
Mawenzi, mtu mmoja aitwaye Richard Shukuru Mwaikimba (26) naye alipigwa
risasi na kufa baada ya kujaribu kumsaidia mfanyabiashara mmoja wakala
wa mitandao ya fedha ya simu za mikononi, aliyevamiwa na majambazi hao
wapatao watatu.
Ilidaiwa kuwa Richard na wenzake
walishuku kuwepo kwa uporaji dukani kwa Tatu, hivyo wakajikusanya ili
kwenda kusaidia, lakini walipokaribia, jambazi mmoja alichomoa bastola
na kumpiga marehemu kabla ya wote watatu kupanda pikipiki moja na
kutokomea kusikojulikana baada ya kupora fedha.
Marehemu ambaye alikuwa mwenyeji wa
Bukoba, na aliyetarajiwa kuzikwa Dar wiki hii, aliwahishwa hospitalini
Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini alifariki muda mfupi baada
ya kufikishwa.
Katika tukio lingine, majambazi
waliokuwa na bastola, walivamia na kupora mamilioni ya fedha katika baa
ya Mawela iliyopo Sinza baada ya kuwalazimisha watu kutoa fedha na simu
walizokuwa nazo wakati wakinywa huku wakitazama mpira.
Mlinzi wa baa hiyo, Peter Otieno Ochola,
akiamini amejificha, alijaribu kupiga simu Polisi ili kuomba msaada,
lakini majambazi hao walimuona na kumpiga risasi ya kichwani
iliyosababisha mauti yake.
Meneja wa baa hiyo, Steven Richad
alisema kwamba majambazi hao walifika katika eneo hilo wakiwa na
pikipiki nne na kufyatua risasi wakiwataka walale chini na kila mmoja
atoe simu na fedha alizokuwa nazo.
“Siku hiyo watu walijaa sana kwa vile kulikuwa na mpira, walichukua vile walivyovitaka na hata huku kaunta waliingia na kupora zaidi ya shilingi milioni tatu, deki na lap top,” alisema.
“Siku hiyo watu walijaa sana kwa vile kulikuwa na mpira, walichukua vile walivyovitaka na hata huku kaunta waliingia na kupora zaidi ya shilingi milioni tatu, deki na lap top,” alisema.
Shukulu.
Kana kwamba haitoshi, amani na utulivu
umeendelea kuwa tete jijini Dar es Salaam, baada ya dada mmoja
aliyefahamika kwa jina la Gloria Uroki, naye kuuawa kwa kupigwa risasi
kichwani mchana wa Jumatatu iliyopita, baada ya majambazi hao kumshuku
kuwa alikuwa akiwasiliana na polisi kuhusu tukio lao.
Tukio hilo lilitokea Kinondoni Morocco
baada ya majambazi hao waliokuwa wanne, kumfuatilia mwanamke mmoja
aliyekuwa amepanda daladala kutoka kusikojulikana. Mara baada ya
kushuka, kijana mwingine naye alishuka kutoka katika gari hilo na
kumtaka kumkabidhi mkoba huo, alipokataa alitolewa bastola na hivyo
kumkabidhi.
Lakini baada ya kuporwa mkoba huo,
mwanamke huyo alianza kupiga mayowe yaliyosababisha majambazi hao
waliokuwa na pikipiki mbili kuanza kukimbia. Akiwa hajui hili wala lile,
Gloria alikatisha barabara akizungumza kwa simu yake ya mkononi.
Wakiwa
wametaharuki, majambazi hao walipomuona na simu sikioni, waliamini
alikuwa akiwasiliana na polisi hivyo kumfyatulia risasi zilizosababisha
kifo chake, miezi mitatu tu baada ya kufunga ndoa.
Wananchi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili wameilaumu serikali kwa kushindwa kudhibiti ongezeko kubwa la silaha aina ya bastola, kwani hivi sasa ni nyingi mithili ya simu za mikononi.
Wananchi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili wameilaumu serikali kwa kushindwa kudhibiti ongezeko kubwa la silaha aina ya bastola, kwani hivi sasa ni nyingi mithili ya simu za mikononi.
tiko
tiko
Post a Comment