tiko
tiko
Mama mmoja, Sara Zoya mkazi wa Mabibo Makuburi, jijini Dar es Salaam amekimbilia polisi na kudai kuwa watoto wake walitekwa na ndugu yake kisha kupelekwa kusikojulikana baada ya kufukuzwa kwenye nyumba yao ya familia.
Sara alidai kuwa ndugu yao huyo
aliyefanya kitendo hicho cha utekaji ni Hilda Zoya ambaye anadai
aliwateka watoto Imani (14) na Leila (5).
Akizungumza na gazeti hili Sara alisema,
alikuwa akiishi na mumewe na baada ya kuachika kwa mume wake aliamua
kurudi kwao kwenye nyumba ya familia na watoto hao wawili. Aliendelea
kufafanua:
“Sisi tulizaliwa watoto sita kwa baba na
mama mmoja na mimi ndiye mtoto wa kwanza na wazazi wetu wote
walishafariki dunia. Mimi nilipoachika niliwataarifu ndugu zangu kuwa
nataka kurudi nyumbani kwetu Mabibo lakini baadhi yao wakanishauri
niende nikakae Tabata Kisukuru kwenye nyumba ya mdogo wangu anayeishi
Ulaya.
“Mimi sikupenda, nikakataa nikaenda
kuishi kwetu, ilipofika Desemba 17 mwaka huu, ndugu yangu Rachel kutoka
Ulaya aliyekuja likizo aliniomba nimsindikize kwa mjomba anayeishi Mbezi
Beach huku nyuma mdogo wangu Hilda alihamisha vyombo vyote na
kuwachukuwa watoto na kuwapeleka kusikojulikana.
“Niliporudi nyumbani nilikuta milango imefungwa na vitasa vimebadilishwa na kuwekwa mlinzi pia watoto wangu wawili sikuwakuta.
“Niliporudi nyumbani nilikuta milango imefungwa na vitasa vimebadilishwa na kuwekwa mlinzi pia watoto wangu wawili sikuwakuta.
“Nikaenda kwa mjumbe, mwenyekiti wa
serikali za mitaa kuwaarifu na baada ya hapo nikaenda kutoa taarifa
kwenye Kituo cha Polisi cha Mwongozo kilichopo External, wakaniambia
nisubiri kwa muda wa saa 24 lakini sikuwaona wanangu na mama yao mdogo
Hilda alikuwa hapatikani kwenye simu, ndipo nikaamua kurudi tena
kituoni hapo na kufungua kesi kuhusu kutoonekana kwa watoto, vitu vyangu
na mimi kukosa pa kulala.”
Sara amemfungulia kesi mdogo wake Hilda
kwa jalada namba MWP/RB/1655/2014 UTEKAJI WA WATOTO NA WIZI hivyo
anasakwa na polisi.Akifafanua zaidi mama huyo alisema: “Siku ya pili
watoto walirudi wenyewe na walipohojiwa walidai walipelekwa Kinondoni
kwa Manyanya na mama yao mdogo na kutelekezwa huko na aliwaachia
shilingi elfu tano.
“Watoto walisema walipoamka asubuhi
waliwauliza wapangaji wa nyumba hiyo wapi walipo na wakaelekezwa kuwa
pale ni Kinondoni kwa Manyanya.”
Mtoto Imani alipoulizwa na gazeti hili
alikiri kuchukuliwa na mama yao mdogo na kutelekezwa Kinondoni. “Asubuhi
tuliwaomba wapangaji watuelekeze namna ya kufika stendi, tukapelekwa
tukapanda basi mpaka Makumbusho kisha tukafika nyumbani, tukaelezwa kuwa
mama alilala kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa.”
Sasa Sara anaomba msaada wa kisheria
kwani alidai yeye pamoja na watoto wake hawana nguo, vyombo na sehemu
ya kuishi baada ya kufanyiwa unyama huo na mdogo wake huyo na sasa
wamefadhiliwa na mwenyekiti wa serikali za mtaa wanakoishi.
tiko
tiko
Post a Comment