tiko
tiko
Governing
Council of the Party for Democracy and Development (Chadema) Tanga
Region, leading limewasimamisha Chairman, Secretary and members of the
party Handeni District for allegedly failing to take responsibility
within the party as well.
Likewise, the council has taken action similar to that party secretary of Muheza district.
Baraza
la Uongozi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa
Tanga, limewasimamisha uongozi Mwenyekiti, Katibu na wajumbe wa chama
hicho Wilaya ya Handeni kwa madai ya kushindwa kuwajibika ndani ya chama
pamoja.
Kadhalika, baraza hilo limechukua hatua kama hiyo kwa katibu wa chama hicho wilayani Muheza.
Akielezea
hatua hiyo, Katibu wa Chadema mkoani Tanga, Ismail Masoud, alisema
uongozi wa chama hicho umewasimamisha kazi viongozi hao hadi uchunguzi
dhidi yao utakapomalizika.
Aliwataja
viongozi hao kuwa ni Jadi Bamba, ambaye ni Mwenyekiti, Ibrahim Ramia
(Katibu) pamoja na wajumbe sita wa Baraza la Uongozi.
Alisema
viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kushindwa kukisaidia Chama
kunyakua nafasi za uenyekitiwa serikali za mitaa uliofanyika hivi
karibuni na kuunda makundi ndani ya chama hicho.
“Baraza
la Uongozi Chadema Mkoa, limepitisha uamuzi mmoja wa kuwasimamisha kazi
Mwenyekiti, Katibu na wajumbe wote wa wilaya kwa tuhuma za kukihujumu
Chama,” alisisitiza.
Alifafanua kuwa viongozi hao wamesimamishwa hadi uchuguzi dhidi ya tuhuma zao utakapokamilika.
Masoud
alisema kutowajibika kwa makatibu kumesababisha kutoa mwanya kwa vyama
pinzani kujiimarisha na kuchukua maeneo ambayo tayari yalikuwa na
ushawishi mkubwa wa Chadema na kuwa na uhakika katika uchaguzi mkuu ujao
kufanya vizuri nafasi za udiwani.
tiko
tiko
Post a Comment