tiko
tiko
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo
Member
of the Board of Trustees of the Association for Democracy and
Development (Chadema) and Member of Moshi, Philemon Ndesamburo, has
planned to submit a motion in parliament, he urged the Ministry of
Interior of the State, provide information about police failure to
arrest four suspects of murder the intent of the former manager of a
popular pub in here, James John.
Mjumbe
wa Baraza la Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, amepanga kuwasilisha hoja
binafsi bungeni, akiitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kutoa
maelezo kuhusu Jeshi la Polisi kushindwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa
mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa meneja wa baa moja maarufu mjini hapa,
James John.
James
aliuawa Juni 06, mwaka 2009 na watu wanne wanaodaiwa kuwa ndugu wa
familia moja, huko katika Kijiji cha Kindi-Kibosho, Wilaya ya Moshi.
Jana,
Ndesamburo alisema katika hoja yake atamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mathias Chikawe, kulieleza Bunge sababu zinazolifanya Jeshi la
Polisi kushikwa na kigugumizi cha kuwakamata watuhumiwa hao na
kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
“Katika
maelezo ya hoja hiyo, nitataka pia serikali kueleza lilipo jalada la
uchunguzi wa mauaji hayo. Nimeamua kuchukua uamuzi huu, kwa kutumia
Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977, ambayo imelipa Bunge, Mamlaka ya kuishauri na kuisimamia Serikali
na vyombo vyake katika kutekeleza majukumu yake,” alisema Ndesamburo.
Alisema
yeye kama Mbunge wa Moshi Mjini, ambaye amekuwa akiheshimu utawala wa
sheria, ameamua kulichukua jambo hilo na atalipeleka bungeni baadaye
mwezi huu ili kulisukuma Jeshi la Polisi liwajibike kutekeleza wajibu
wake.
Jeshi
la Polisi liliwakamata na kuwafungulia mashtaka ya mauaji, watu wawili
tofauti (Majina yao yamehifadhiwa), ambao hata hivyo, waliachiwa huru na
Mahakama baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), kudai hakukuwa
na ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani watuhumiwa hao.
Wakati,
Ndesamburo akijitwisha msalaba huo, baadhi ya ndugu wa marehemu James
wamemwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu, kuingilia
kati sakata hilo ili kutoa msukumo utakaopelekea kukamatwa kwa
watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo.
tiko
tiko
Post a Comment