tiko
tiko
JESHI
la polisi mkoani Mara, linamsaka Simion Otieno,baada ya kudaiwa kuchoma
nyumba kwa kutumia mafuta yaa petroli na kusababisha kifo cha
mtoto,Tatu Simion (1).
Tukio
hilo lililotokea Machi 31, mwaka huu katika Kijiji cha Bwai,wilayani
Butiama ambapo chanzo chake kinadaiwa ni wivu wa mapenzi kati ya Otieno
na mama wa mtoto huyo, Kudra Janja ambaye ameunguzwa vibaya mwili mzima.
Janja amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, kwa matibabu zaidi.
Janja amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, kwa matibabu zaidi.
Akizungumza jana, mama mdogo wa Janja,Bahati Magesa, alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mjomba wao saa 10 usiku.
Alisema Januari, mwaka huu,mwanaume huyo pamoja na mke wake walioishi kwa mwaka mmoja,walikuwa na ugomvi kwa muda mrefu.
Alisema Otieno alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano wa mapenzi na watu wengine,lakini baadaye ugomvi huo ulikwisha na waliendelea kuishi vizuri.
“Janja ni mtoto wa dada yangu,mimi naishi mbali kidogo na kwake,jana usiku (juzi) baada ya tukio, alinisimulia kuwa mume wake aliingia ndani akiwa na dumu la petroli na alipomuuliza alimwambia alale.
“Baadaye alichukua kiberiti, huku mkewe akimuuliza mbona unachukua kiberiti usiku huu, akamjibu hayakuhusu, baada ya muda kidogo alitoka nje, akamwaga mafuta dirishani kisha akawasha moto na kukimbia kusikojulikana,”alisema Bahati.
Alisema baada ya kuwashwa moto huo,alipiga kelele na kuomba msaada ndipo mjomba wake Obadia Janja alipomka na kwenda kumsaidia.
“Yaani wakati Obadi anamtoa ndani, tayari alikuwa ameungua vibaya na mtoto alikuwa ameumia mno,”alisema Bahati.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wameanza kumtafuta muhusika.
Alisema tukio hilo, ni la kinyama na linapaswa kulaaniwa na kila mmoja na kuiomba jamii kuacha kujichukuliwa sheria mkononi.
tiko
tiko
Post a Comment