tiko
tiko
Mwenyekiti wa ACT, Anna Mghwira
Chama
cha ACT -Wazalendo, kimewataka Watanzania kuipigia kura ya hapana
Katiba inayopendekezwa kwa sababu imeleta mgawanyiko katika taifa
kutokana na kupatikana kwa njia zisizo za kiuadilifu na mchakato wake
kuendeshwa kibabe.
Kadhalika,
kimesema katiba hiyo haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye
masuala ya mbalimbali, ikiwamo muundo wa serikali, miiko na maadili ya
viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya Rais na uwiano wa
muhimili wa dola.
Mwenyekiti wa ACT, Anna Mghwira, alisema jana kwa waandishi wa habari, kuwa:
“Suala
la Katiba, tumeamua kuwa tutaanza nalo mara ya kukamata dola, tutaanzia
pale alipoishia Jaji Joseph Warioba, hii inatokana na ukweli kwamba
mchakato wa uundaji wa Katiba mpya ulifanywa batili na hatua
zilizofuatwa baada ya rasimu ya pili kukamilika.”
Anna,
alisema azimio lingine la mkutano wa Kamati Kuu ni kumuagiza Katibu
Mkuu wake, Samson Mwigamba, kutangaza nafasi ya kuwapata wajumbe
watakaoingia kwenye kamati ya uadilifu ya chama taifa, mchakato ambao
utaanzia ngazi za chini za chama.
tiko
tiko
Post a Comment