tiko
tiko
Mohammed Mdose na Khadija Mngwai
Dar es Salaam
KLABU ya Yanga imehoji juu ya uwepo wa kiongozi mmoja ndani ya Bodi ya Ligi huku akiwa na wadhifa mwingine kwenye klabu pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kusema kuwa hiyo ni moja ya kulifanya soka letu lizidi kudorora.
Dar es Salaam
KLABU ya Yanga imehoji juu ya uwepo wa kiongozi mmoja ndani ya Bodi ya Ligi huku akiwa na wadhifa mwingine kwenye klabu pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kusema kuwa hiyo ni moja ya kulifanya soka letu lizidi kudorora.
Japo Yanga hawakumtaja moja kwa moja kiongozi huyo, lakini habari
zinadai kuwa kiongozi huyo ni Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange
‘Kaburu’ ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF pamoja na
Mjumbe wa Kamati ya Kujadili Matukio ya Ligi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema kuwa Yanga inashangaa kumuona
kiongozi huyo akiwa na ‘kofia tatu’ kwenye taasisi kubwa za soka hapa
nchini kitu ambacho hakifanyiki popote pale duniani.
Alisema kuwa uwepo wa kiongozi huyo pamoja na viongozi wengine ambao
hawana sifa za kuliongoza soka la Tanzania ni bora wawaachie wenye sifa
ili soka letu likue.
“Hatuna imani na Bodi ya Ligi kwa jinsi inavyoendeshwa, umeona wapi
kiongozi mmoja ana vyeo vitatu tofauti ndani ya TFF, Bodi ya Ligi, TFF
pamoja na klabu? Bora wawaachie wengine ambao wana vigezo vya kukaa
kwenye chombo hicho na siyo wao, lazima tuhoji vigezo vilivyowafanya
wapewe nafasi hizo tunafikiri siyo sawa kwa mtu huyo kuwa na vyeo
hivyo,” alifafanua Muro wakati wa mkutano na waadishi wa habari jijini
jana.
Yanga chini ya Mwenyekiti wake Yusuf Manji na Makamu Clement Sanga,
imekuwa ni timu yenye msimamo mkali sana pale inapoona kuwa hakuna haki
kwenye jambo fulani.
Yanga imekuwa ikiamini kuwa kiongozi huyo ambaye ana nguvu kubwa amekuwa
akitumia cheo chake kuvuruga baadhi ya mambo ili kuona Yanga hawapati
haki yao hivyo wanataka aachie baadhi ya nyadhifa zake ili haki
ipatikane kwenye maamuzi ya kamati hizo.Hata hivyo, Championi lilifanya
jitihada za kumtafuta kiongozi huyo lakini ziligonga mwamba.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment