tiko
tiko
WAKATI Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwasili mjini Shinyanga kwa ajili ya kujionea maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa ya mawe katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilaya ya Kahama, idadi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia 42 na idadi ya majeruhi ni 98.
Pinda baada ya kuzuru eneo la tukio, aliwaahidi waathirika wa tukio hilo kuwa Serikali itawasaidia kwa kadiri itakavyowezekana.
Mpaka jana asubuhi majeruhi 98 walikuwa bado wamelazwa katika
Hospitali ya wilaya ya Kahama na wengine zaidi ya 600 hawana mahali pa
kuishi kufuatia kuezuliwa kwa mapaa na kubomoka kwa nyumba 160.
Mvua hiyo iliambatana na upepo mkali na mawe makubwa pamoja na vifo
vya watu. Madhara mengine ni pamoja na kuangamia kwa mamia ya mifugo
wakiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku na mamia ya ekari za mazao mbali
mbali.
Huku misaada ya huduma muhimu za jamii kwa waathirika kama chakula
ikihitajika kuna uwezekano wa kuzuka kwa magonjwa ya milipuko.
Juzi viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally
Rufunga, kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha na vikosi
vya uokoaji yakiwemo magari ya wagonjwa yalifika eneo la tukio kutoa
misaada .
Wakati huo huo Chama cha Wananchi (CUF) kimetuma salamu za rambirambi
kwa familia zilizofiwa na ndugu zao kutokana na mafuriko yaliyoikumba
wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga juzi.
Katika taarifa ya salamu za rambimbi za chama hicho iliyotolewa na
Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Shaweji Mkweto, amezitaka familia hizo kuwa na
utulivu katika kipindi hiki cha maombolezo ya ndugu zao.
Mketo alisema, chama hicho kimesikitishwa na tukio hilo, ambapo
alisema kwa uchunguzi walioufanya walibaini kuwa madhara hayo makubwa
yanatokana na miundombinu ya mikondo ya maji kutorekebishwa ili kuzuia
mafuriko.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria Limbe ambao
wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na mawe
iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi 3 usiku. Alikwenda katika
maeneo yaliyoathirika kuwapa pole wananchi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro ambaye ni mmoja wa majeruhi
wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha
kwenye eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku.
Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa
pole majeruhi waliolazwa hospitalini hapo
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu,
Jenista Mhagama (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr Rufunga kukagua
maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na mawe
katika eneo Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment