tiko
tiko
Kwa
kuzingatia ushahidi na utetezi wa pande zote jaji Joaquine De-mello
amesema mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka yoyote kuwa
watuhumiwa wote wanne walihusika na mauaji ya Bi Zawadi Magindu katika
kijiji cha Nyamalulu wilayani Geita mnamo tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka
2008 usiku.
Kwa
mujibu wa mashahidi waliojitokeza inasemekana mtuhumiwa namba mbili
Ndahanya Lumola na mtuhiwa namba tatu Singu Siantemi ndio waliohusika na
upimaji wa mifupa ya marehemu Zawadi ambapo hutumia wembe na shilingi
moja kuweka karibu na mifupa ya Albino ili kujua kama itavuta kama
sumaku na kipimo kingine ni redio ambayo huiweka karibu na mifupa na
ikizimika ndio mifupa hiyo huonekana kuwa na ubora tofauti na hapo
mifupa hiyo huwa haifai na hutupwa.
Mashahidi hao wamesema vipimo hivyo havina uhalisia wa aina yoyote kwani hakuna binadamu mwenye mifupa inayokuwa na sumaku.
Aidha
jaji De-mello amesema anashangazwa na kesi zote alizosimamia zinazohusu
mauaji ya Albino watuhumiwa wote wanaofikishwa mahakamani ni wakataji
wa mapanga na kuhoji wakataji hao wanapeleka wapi mifupa hiyo? Na
kuwataka wahusika kuhakikisha wanawapata wanunuzi na watumiaji wa viongo
hivyo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Watu
waliokutwa na hatia ya kufanya mauaji hayo ni Masalu Kahindi, Ndahanya
Lumola, Singu Siyantemi na Nassoro Saidi ambaye ni mume wa marehemu
Zawadi.
Kwa
upande wao watu wenye ulemavu wa ngozi wameipongeza mahakama kwa kutoa
hukumu ya haki inayoashiria kuwapa ulinzi jamii hiyo ya maalbino.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment