tiko
tiko
Hii bado ni story ambayo imeendelea kukaa kwenye headlines, siku chache zimepita tangu Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aanguke kwenye ngazi akiwa anashuka baada ya kuhutubia wananchi na wanachama wake.
Story ziliendelea mitandaoni kuijadili
ishu hiyo, watu wa graphics nao wakatengeneza picha mbalimbali za
kuchekesha kitu ambacho kiliwakwaza viongozi wa chama cha ZANU-PF.
Leo vyombo vya habari Zimbabwe
vimeripoti kuhusu Rais huyo kuwatimua kazi wafanyakazi 27 kwenye kikosi
cha Usalama kwa kushindwa kuwajibika wakati Rais huyo akianguka.
Uzembe ambao unaonekana kufanywa na
jamaa hao ni kitendo cha kushindwa kumdaka kiongozi huyo wakati
akianguka, kibaya zaidi ni kwamba alianguka mpaka chini bila msaada
wowote kutoka kwao huku wakiwa wamesimama pembeni yake.
Vingine ambavyo huenda hatukuwahi
kuvisikia kuhusu ishu hii ni kwamba waandishi waliopiga picha wakati
Rais huyo akianguka walilazimishwa na walinzi wa Rais kufuta picha hizo.
Taarifa za kutoka Ikulu ya Rais huyo
zinasema huu ni mwanzo tu, uchunguzi unaendelea na wakipatikana wazembe
wengine nao watawajibishwa kama walivyofanyiwa hapa.
Hii ni video ikionesha Rais huyo wakati akianguka huku walinzi wake wakiwa pembeni yake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment