tiko
tiko
Mahakama
ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, imewahukumu kifungo cha miaka mitano
jela kila mmoja, Joseph Christopher (25) mkazi wa kijiji cha Nkome na
Bahati Juma (28) mkazi wa Katoro wilayani Chato, baada ya kuwatia
hatiani katika shitaka la kujifanya maofisa wa polisi kwa lengo la
kufanya utapeli.
Katika
kesi hiyo, washitakiwa hao walidaiwa kufanya utapeli katika kijiji cha
Buseresere, Septemba 4, mwaka jana na kujipatia simu mbili za mkononi
pamoja na Sh. 11,000 taslimu kinyume cha sheria.
Katika
hati ya mashtaka, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, Alex Mukama,
aliieleza mahakama kuwa, washitakiwa hao walitenda kosa hilo kwa lengo
la kujipatia mali hizo baada ya kujitambulisha ni maofisa wa Jeshi la
Polisi na kwamba wametumwa kijijini hapo kufanya upelelezi wa wahalifu.
Alidai
baada ya kutumia ulaghai huo, washtakiwa hao walichukua simu za mkononi
za vijana wawili pamoja na fedha Sh. 11,000 kisha kutokomea na kuwaacha
vijana hao wasijue la kufanya.
Alieleza
hata hivyo, vijana hao walifanikiwa kumuona mmoja wa washtakiwa hao
akiwa kituo cha mabasi na kuanza kupiga yowe la kuomba msaada, ambapo
alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Buseresere.
Mukama
aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe
fundisho kwa wengine wenye kufanya vitendo vya kulidhalilisha Jeshi la
Polisi na kusababisha wananchi kupoteza imani nalo.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Chato, Jovith Katto,
alisema baada ya mahakama kusikiliza pande zote mbili ya walalamikaji
na walalamikiwa, pasipo shaka mahakama hiyo inawatia hatiani washtakiwa
na kuwahukumu kwenda jela miaka mitano kila mmoja na kwamba iwapo
hawakuridhika na hukumu hiyo wanaruhusiwa kukata rufaa.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment