tiko
tiko
MKAZI wa Kijiji cha Mayaka, Kata ya Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Samaha Mtawa (6) amekufa baada kubakwa na kunyongwa wakati akichuma matunda porini.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi, Thobias
Sedoyeka, mwili wa mtoto huyo ulionekana Februari 7 mwaka huu saa 12
asubuhi umbali wa mita 150 kutoka nyumbani kwao.
"Uchunguzi
wa awali umebaini marehemu alifariki baada ya kubakwa, kunyongwa na
kutupwa porini na mtuhumiwa aitwaye Ramadhani Omari (28), mkazi wa
Maweni," alisema.
Aliongeza
kuwa, uchunguzi huo pia umebaini mbinu ambayo ilitumiwa na mtuhumiwa ni
kumvizia marehemu akiwa anachuma matunda hivyo alimkamata kwa nguvu na
kumfanyia unyama huo.
Kamanda
Sedoyeka alisema licha ya marehemu kupiga kelele na wananchi kukimbilia
eneo hilo ili kumwokoa, walipofika walikuta tayari amefariki na
mtuhumiwa kakimbia lakini alikamatwa baada ya saa mbili.
"Jeshi
la Polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa upelelezi zaidi na baada ya
kukamilika, atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili, mwili wa
marehemu ulifanyiwa uchunguzi na daktari na baadaye kukabidhiwa ndugu
zake," alisema.
Amewahadharisha
wazazi na walezi wa watoto kutowaachia ovyo watoto wao na kucheza
katika mazingira salama ili wasiweze kufanyiwa vitendo vya kikatili kama
ubakaji na mauaji jambo ambalo linaleta simanzi na majonzi.
Wakati
huo huo, wananchi mkoani humo wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya
makundi ya kigaidi yaliyoanza kuingia nchini, kujihusisha na vitendo
vinavyoleta uvunjifu wa amani kwa jamii na Taifa.
Wito
huo ulitolewa jana na Kamanda Sedoyeka baada ya kukamatwa baadhi ya
watuhumiwa kwenye maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kujihusisha na
matukio ya ugaidi ukiwemo wa ulipuaji mabomu na mauaji ya raia.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment