tiko
tiko
Mtu mmoja amekamatwa akiwa anasafirisha
bangi baada ya gari alilokuwa akisafirishia kupata ajali likiwa
linatokea maeneo ya Busya kuelekea Nairobi, Polisi wakafanikiwa
kumkamata mtuhumiwa huyo.
“Bangi
sio kitu ngumu hata tumbaku ni so expensive kushinda bangi… sasa bangi
ngoja nikuambie hiyo tani moja tukinunua Uganda ama Tanzania tunanunua
50 buku na tunauza 100 buku, lakini saa hii hawa wakikushika wanakuambia
one milion, sasa one milion ningekuwa nafanya hii kazi? Ningepata one
milioni kwani mimi nitakuwa mjinga nikimbie njiani kila siku?“– alijitetea mtuhumiwa huyo.
Mtuhumiwa huyo ambaye amepelekwa rumande
amekiri kufanya biashara hiyo kwa zaidi ya miaka kumi sasa likiwa ni
tukio lililotokea siku chache baada ya watuhumiwa wengine kukamatwa na
bangi katika maeneo hayo.
Unaweza kuisikiliza taarifa hiyo kutoka kituo cha K24 hapa.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga
na mimi
tiko
tiko
Post a Comment