tiko
tiko
FAMILIA za Bobby Brown na marehemu Whitney Houston zimekubaliana
kumwondolea Bobbi Kristina mashine inayomsaidia kupumua kesho, Jumatano
ili afe tarehe sawa na ile ambayo mama yake mzazi, Whitney Houston
alifariki.
Mjukuu wa Bobbi, Cissy Houston alitoa wazo hilo la Februari 11 wakati wa
majadiliano yaliyofanyika wikiendi iliyopita kati ya familia ya Whitney
Houston na Bobby Brown kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory huko
Atlanta nchini Marekani.
Brown alitoa baraka zake kuruhusu binti yake huyo aondolewe mashine ya
kupumua wakati wa usiku ili afe tarehe moja ya Februari 11 sawa na mama
yake aliyefariki Februari 11, 2012 katika Hoteli ya Beverly Hilton.
Maamuzi hayo yamefikiwa ili kuweka kumbukumbu ya mama na binti yake ili wote wapumzike kwa amani, familia ya Brown ilieleza.
Bobbi Kristina, 21, binti pekee wa Houston na mwimbaji Bobby Brown,
amepoteza fahamu tangu alipokutwa bafuni hakiwa hajitambui Januari 31,
mwaka huu.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment