tiko
tiko
WATOTO wa
bondia bingwa wa dunia anayetambuliwa na shirikisho la WBE, Francis
Cheka aliye gerezani, wamemliza babu yao, Boniface Cheka ambaye ni baba
mzazi wa mwanamasumbwi huyo wakati alipowatembelea nyumbani kwao, kwa
mara ya kwanza tangu kutolewa kwa hukumu hiyo wiki mbili zilizopita.
Mzee huyo ambaye makazi yake yako Dar es Salaam alifika mjini hapa kwa
mara ya kwanza tangu mwanaye ahukumiwe, akiwa ameongozana na ujumbe
kutoka Shirikisho la Ngumi la TPBO chini ya Rais wake, Abdalah Ustaadh.
Ujumbe huo ulifika mjini hapa Jumapili iliyopita na kwenda moja kwa moja
katika gereza la Manispaa alikofungwa bondia huyo, ambako baada ya
kumsalimia, walikwenda nyumbani kwake, ambapo baada ya kuwaona watoto na
mkewe, mzee huyo naye alijikuta akishindwa kujizuia na hivyo kuangua
kilio.
Awali wakiwa gerezani hapo, msafara huo ulishuhudia umati mkubwa wa
mashabiki waliofika kwa ajili ya kumuona bondia huyo kipenzi chao,
aliyefungwa kwa kosa la kumpiga ngumi meneja wa baa yake. Hata hivyo,
wengi wa watu hao walikataliwa kumuona.
Rais wa TPBO, Ustaadh, alisema walikuja mjini hapa wakiwa na mwanasheria
wao, ambaye amewaambia kuwa watalazimika kwanza kufika mahakamani ili
kujua hatua za kuchukua, katika harakati za kutaka kumtoa hatiani,
bondia huyo aliyekuwa kipenzi cha wengi.
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI KUHUSU HABARI HII
tiko
tiko
Post a Comment