tiko
tiko
Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
WATU zaidi ya 50 wamefariki dunia huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada
ya basi la abiria kugongana na lori la mafuta kisha magari yote
kuteketea kwa moto jirani na Mji wa Karachi nchini Pakistan.
Imeelezwa kuwa lori la mafuta lilikuwa katika spidi kali lilipogongana uso kwa uso na basi hilo.
Basi lilikuwa limebeba watu zaidi ya 60 na lilikuwa likielekea kwenye Mji wa Shikarpur kutokea Karachi.
Dk. Seemi Jamali, mkuu wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Jinnah
mjini Karachi amesema kuwa wamepokea miili ya watu 57 huku akiongeza
kuwa idadi inaweza kuongezeka.
Chanzo: BBC
Kupata Habari Na Matukio Ya Kila Siku Like Page Yetu
tiko
tiko
Post a Comment