tiko
tiko
Kuna
uwezekano mkubwa kama uliikosa hii show kuna vitu vingi umevikosa,
ilikuwa ni show ambayo kila wimbo uliokuwa ukiimbwa, mashabiki walikua
wakiupokea kwa furaha, huenda iliwakumbusha wakati Wateule yote wakiwa kwenye jukwaa moja miaka mingi iiliyopita.
Jaffarie, Mchizi Mox, Jay Moe na Solo Thang waliamua kujikusanya na kuweka nguvu moja kama Wateule kwa kupiga show kali Maisha Club usiku wa January 18.Usiku huu ulitawaliwa na hit songs kama Watu Kibao, Niko Busy, Bishoo, Mvua na Jua, Kama Unataka Demu, Mambo ya Pwani, Vina Utata, Mambo Vipi, Mikasi, Miss Tanzania na zingine kibao.
Hakuna Story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter, instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment