tiko
tiko
Polisi nchini India imemfungulia kesi ya mauaji mwanaume mmoja Abul Hussain kwa kosa la kujaribu kumzika mwanaye wa kike mwenye miaka tisa akiwa hai baada ya kuchukizwa kupata mtoto wa kike.Tukio hilo liliripotiwa na majirani wa baba huyo baada ya kuona akimzika mwanaye nyuma ya nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Sipaijala na kuamua kupiga simu polisi kuomba msaada.
“Tuliona akimfunga mikono kisha kumziba mdomo na baadaye kumfukia hadi usawa wa kichwa huku mtoto huyo akijaribu kujiokoa bila mafanikio,” alisema mmoja wa majirani.
Baada ya askari kufika walimwokoa mtoto huyo na kumkimbiza hospitali ambapo inasemekana hali yake bado ni mbaya na wakati wa tukio mama yake hakuwepo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment