Realtime blog statistics Realtime blog statistics
Scanning..

Boss alibebwa na wakulima ili viatu visiharibike kwenye barafu, kilichofuatia ni story!

tiko tiko
Mr. Ofisa II
Picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii Uturuki zikimuonyesha kiongozi wa Idara ya Huduma Vijijini akiwa amebebwa juu na wakulima ili kukwepa barafu zilimponza, ikaamriwa asimamishwe kazi.
Afisa huyo, Nedim Zunarci alionekana amebebwa na wakulima hao katika Jimbo la Manisa wakati akikagua athari zilizosababishwa na barafu aliyoanguka kutokana na baridi kali, akahofia viatu vyake vitaharibika kutokana na barafu hiyo, hivyo akabebwa na wakulima hao.
Meya wa Manisa, Cengiz Ergun alisema kitendo hicho hakiendani na utaratibu wa kazi wala maadili, pia hakionyeshi uhusiano mzuri kati ya viongozi na jamii.
Mr. Ofisa
Comments za watu kwenye mitandao ya kijamii Uturuki walionekana kukosoa pia kitendo hicho baada ya picha hiyo kuzagaa.
Unahitaji kupata kila stori inayonifikia mtu wangu? Ni rahisi sana, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko tiko

Post a Comment

CodeNirvana
© Haki Zote Zimeifadhiwa Kalamu 1 | designed by tabasamu na ∂αиιєℓι
Code Nirvana
Back To Top