tiko
tiko
Jambo limezua jambo!
Siku chache baada ya kuripotiwa kwa tukio la staa wa sinema za Kibongo,
Wema Isaac Sepetu kunaswa kimalovee na Rais wa Masharobaro, Raheem
Rummy Nanji ‘Bob Junior’, mwigizaji chipukizi, Bozi ameibuka na kudai
‘Wema niachie Bob Junior wangu’.
Mwigizaji chipukizi katika tasnia ya filamu Bongo, 'Bozi' akihuzunika.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada
ya habari hiyo kuruka hewani kupitia gazeti tumbo moja na hili, Amani la
wiki iliyopita, mrembo huyo alipoziona picha za wawili hao alipoteza
fahamu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda huku akiangua kilio, Bozi alisema kuwa katika siku alizowahi kuumia ni siku hiyo alipoona Wema ametoka kwenye gazeti na mpenzi wake huyo.
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu akiwa mapajani mwa 'Bob Junior'.
Bozi alifunguka kwamba, alimbana Bob Junior kwa maswali lakini jamaa huyo hakutaka kumweka wazi kama yeye na Wema wanatoka.
tiko
tiko
Post a Comment