tiko
tiko
Ni mara chache tumesikia viongozi wakubwa kwenye nafasi kama Rais akiomba radhi hadharani hata kama ni kweli amekosea.
Moja ya video zilizopata umaarufu mkubwa
ndani ya saa chache ni hii inayoonyesha bibi na bwana wakiwa kwenye
suti na shela, kwenye pilika pilika za sherehe ya ndoa kisha ikapigwa
simu kutoka kwa Rais Obama akiwaomba maharusi hao radhi kwa kuwahamisha
sehemu ambayo ilikuwa sherehe ya wawili hao ifanyike.
Maafisa usalama wa Marekani walilazimika
kuwahamisha maharusi hao katika eneo ambalo ilikuwa ifanyike sherehe
yao kwa kuwa Rais Obama alikuwa akienda kucheza gofu katika kipindi cha
mapumziko.
Maharusi hao ambao wote ni wanajeshi, Kapteni Hiemel na Kapteni Mallue walipokea
simu kutoka kwa Obama akiwaomba radhi kwamba alichelewa
kupatiwa taarifa kuhusu shughuli ya maharusi hao kufanyika katika
viwanja hivyo.
Hii ni video inayoonyesha maharusi hao wakiongea na Rais Obama.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi
tiko
tiko
Post a Comment