tiko
tiko
Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’ ambaye pia alishawahi kunyakua taji la Miss Tanzania 2001, ‘amemsapraiz’ mwanamitindo na mbunifu Jokate Mwegelo, kwa kumpatia keki yenye sura ya mdomo wake.
Awali, kulikuwa na kikao cha kawaida cha
kujadili mambo mbalimbali ya kikazi baina yao kilichofanyika ndani ya
hoteli ya Hyatt Kempisky, iliyopo Posta Jijini Dar, lakini kumbe Millen
alikuwa ameandaa keki.
“Yaani mimi nilijua tunakutana kama
tulivyopanga, lakini cha kushangaza nikakuta watu wakiongozwa na dada
yangu Millen wameniandalia keki mbalimbali ikiwemo moja kama mdomo wangu
kabisa na kidoti juu, kwa kweli nilifurahi sana siwezi kuelezea,”
alisema Jokate.
tiko
tiko
Post a Comment